TANGAZO KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2023/2024 KATIKA KAMPASI ZA DAR ES SALAAM, TABORA, MTWARA, SINGIDA, TANGA, MBEYA


Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo katika ngazi ya Cheti na Diploma kwa kada tofauti zinazotolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania katika Kampasi zake za Dar es Salaam, Tabora, Mtwara, Singida, Tanga na Mbeya katika udahili wa Oktoba kwa mwaka wa masomo 2023/2024 wanatakiwa kuzingatia maelekezo muhimu yafuatayo.

1. Kuwasili Chuoni

Wanafunzi wanapaswa kuwasili Siku ya Jumatatu tarehe 09 Oktoba, 2023 kwa wiki ya maelekezo na usajili kwa wanachuo. Mwanafunzi atakayeripoti baada ya tarehe 27 Oktoba 2023 hatapokelewa.

2. Vitu vinavyohitajika:

Wanafunzi wote wanapaswa kuja na

i.Kwa wale wa ngazi ya Cheti:

Vyeti halisi na nakala mbili za: Cheti cha kuzaliwa, Cheti cha kuhitimu kidato cha Nne au cha matokeo (Result Slip kwa wahitimu wa mwaka 2022), Picha tatu za pasipoti zinazofanana.

ii.Kwa wale wa ngazi ya Diploma:

Cheti cha kidato cha IV na kidato cha VI au Cheti cha NTA Level 4. Picha tatu za pasipoti zinazofanana.

3. Fomu ya maelekezo ya kujiunga:

Tafadhali pakua fomu ya maelekezo ya kujiunga na Chuo kwenye tovuti ya Chuo ambayo ni www.tpsc.go.tz au fika chuoni kupata barua yako.

4. Malipo ya Ada

Malipo ya ada yafanywe mapema kabla ya tarehe 9 Oktoba, 2023 kwa kutumia “Control number” kutoka kwenye ofisi za uhasibu Chuoni. Kwa mawasiliano tumia namba za simu zilizopo kwenye Fomu ya kujiunga na Chuo.

NB: Chuo kimeanza kupokea maombi ya awamu ya pili kwa kampusi zote hadi tarehe 20 Septemba, 2023.