MAHAFALI YA 38 YA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA TANZANIA (TPSC)


Kaimu Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania anapenda kuwatangazia wahitimu wote na wadau wa Chuo cha Utumishi wa Umma kwa ujumla kuwa Mahafali ya Thelathini na Nane (38) kwa Kampasi zote za Chuo cha Utumishi wa Umma yatafanyika siku ya Ijumaa , tarehe 24 Novemba 2023 katika viwanja vya Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora, kuanzia saa tatu (03.00) asubuhi.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Mhe. George B. Simbachawene (MB).

Majina ya wahitimu yanapatakana kwenye tuvuti ya Chuo (www.tpsc.go.tz).

Aidha, wahitimu wote wanahimizwa kuhudhuria mahafali hayo. Mazoezi (Rehearsal) yatafanyika siku ya Alhamisi tarehe 23 Novemba 2023 katika Kampasi ya Tabora saa nane (08.00) mchana.

Wahitimu wanatakiwa kuvaa suti zinazokubalika Chuoni (nyeusi au dark blue). Gharama ya Joho ni shilingi 30,000 kwa wahitimu wa Shahada ya kwanza na Skafu shilingi 10,000 kwa wahitimu wa Cheti na Stashahada.

Aidha, wahitimu mnatakiwa kuthibitisha ushiriki wenu kupitia namba. 0717152111 /0764775034/0784680077/071757452/0717574525

IMETOLEWA NA:

KITENGO CHA MAWASILIANO NA MASOKO